Yanga wakamia kupata vikombe viwili msimu huu, Mwambusi afafanua mpango mzima
Baada ya kikosi cha Yanga kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (FA), benchi la ufundi la timu hiyo chini ya mkufunzi wake George Lwandamina raia wa Zambia, limeweka hadharani kuwa mipango yao ni kuhakikisha kikosi hicho kinatwaa mataji mawili msimu huu; ligi kuu na Kombe la FA.
Yanga walitinga hatua hiyo baada ya kuiondosha Prisons ya Mbeya kwa mabao 3-0 kwenye mchezo wa robo fainali uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar juzi Jumamosi.
Kocha msaidizi wa timu hiyo, Juma Mwambusi amefunguka kuwa wanataka makombe hayo kwa ajili ya kupooza machungu waliyonayo baada ya kutolewa kwenye michuano ya kimataifa ambako walielekeza nguvu zao msimu huu.
"Nguvu kubwa ilikuwa ni kufanya vizuri kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, lakini kila kitu kiligeuka ndoto baada ya kutolewa, hivyo akili zetu ni kuhakikisha tunachukua makombe yaliyobakia hapa nyumbani.
"Tuna nafasi nzuri kwenye ligi, japo Simba wapo juu yetu kwa sasa, hilo halituogopeshi sana kwani tukishinda mechi zetu za viporo, mambo yatakua sawa, pia tunataka kufanya vizuri katika FA kwa ajili ya kujihakikishia nafasi ya kutinga michuano ya kimataifa msimu ujao," alisema kocha huyo.
Yanga wakamia kupata vikombe viwili msimu huu, Mwambusi afafanua mpango mzima
Reviewed by Steve
on
Monday, April 24, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment