Serikali ilivyoingilia kati suala la Simba na Kagera
Serikali imeingilia sakata la Simba kuhusiana na lile suala la kadi tatu za njano za beki wa Kagera Sugar, Mohamed Fakhi.
Serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT), imesema haifurahishwi na hali inavyokwenda na TFF wanapaswa kulishughulikia.
BMT imetaka TFF kulishughulikia suala hilo kwa uadilifu na haki ipatikane huku ikisisitiza, Simba inapaswa kuwa makini na kuangalia suala la amani na usalama wa taifa.
Hivi karibuni, Simba ilitishia kuandamana ikidai kuna dalili za kutotendewa haki huku ikimlaumu moja kwa moja Rais wa TFF, Jamal Malinzi ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Kagera pia, Jamal Malinzi.
Serikali ilivyoingilia kati suala la Simba na Kagera
Reviewed by Steve
on
Sunday, April 23, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment