Propellerads

Real Madrid wanamtaka Hazard!!??




Imeripotiwa kua klabu ya Real Madrid wako kwenye mpango wa
kujaribu kuongea na Chelsea ili kumnasa Eden Hazard.

Mchezaji huyo mwenye miaka 24 alishinda kua mchezaji bora wa mwaka na kwa mujibu wa Sunday Times , Rais wa Real Madrid Florentino Perez hawezi kuchomoa bei yoyote atakayotajiwa na Chelsea.

Inaaminika kua Los Blancos wanakusudia kumuuza Cristiano Ronaldo kwenda PSG au Gareth Bale kwenda Manchester United kuwezesha dili hilo na pia kumfanya Hazard kuwemo kwenye kikosi cha kwanza.

Hazard amefunga magoli 19 na kutengeneza nafasi 13 katika mechi 53 alizocheza katika michuano yote kwa Chelsea mwaka jana.
Real Madrid wanamtaka Hazard!!?? Real Madrid wanamtaka Hazard!!?? Reviewed by Steve on Monday, September 28, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.