Propellerads

Kuhusu kutimuliwa Mourinho, uongozi wa Chelsea umekuja na hii taarifa


                             Default
Chelsea wametoa tangazo rasmi ambapo wamekanusha
kumfukuza kocha Jose Mourinho.

Fundi huyo kutoka Ureno aliibuka na kudai kua hawezi kuikimbia Chelsea pamoja na matokeo mabovu ya sasa huku akisema hata kama uongozi ukimtimua watajutia kupata kocha bora kama yeye.

Hata hivyo bodi ya klabu hiyo inaonekana kumuunga mkono kocha huyo pamoja na matokeo mabovu ya sasa ambapo wametoa taarifa rasmi kupitia mtandao wa Twitter kumuunga mkono Mourinho

The club wants to make it clear that Jose continues to have our full support... http://che.lc/OGyyNG 

Taarifa hiyo rasmi inasema kua "Klabu inataka kuweka wazi kua tutaendelea kumpa mchango Jose.

"Kama Jose alivyosema mwenyewe, matokeo hayajawa mazuri ya kuridhisha na kiwango cha timu lazima kiboreshwe.

"Hata hivyo tunaamini tuna meneja sahihi kubadilisha hali msimu huu na ana kikosi kitakachofanya hivyo."


Chelsea wameshinda michezo miwili pekee ya ligi msimu huu kati ya nane huku wakiangukia nafasi ya 16 katika msimamo.
Kuhusu kutimuliwa Mourinho, uongozi wa Chelsea umekuja na hii taarifa Kuhusu kutimuliwa Mourinho, uongozi wa Chelsea umekuja na hii taarifa Reviewed by Steve on Monday, October 05, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.