Propellerads

Samatta alivyowapeleka Mazembe fainali ya klabu bingwa Afrika



                        
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta jana amepiga
bao mbili wakati Roger Assale akipiga moja kuipa TP Mazembe ushindi wa goli 3-0 kwenye uwanja wake wa nyumbani jijini Lubumbashi dhidi ya El Merreikh kwenye mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya klabu bingwa barani Afrika hatimaye kutinga hatua ya fainali.

Kiwango kilichooneshwa na klabu hiyo ya Congo kilitosha kabisa kubadili matokeo ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa goli 2-1 uliopigwa Sudan.

TP Mazembe itakuna na USM Alger ya Algeria kwenye mchezo wa fainali ambapo TP Mazembe watasafiri kwenda Algeria kati ya Octoba 30 na Novemba 1 kwa ajili ya mchezo wa awali wakati mchezo wa marejeano ukitarajiwa kupigwa kati ya Novemba 6-8 nchini Congo DR.
Samatta alivyowapeleka Mazembe fainali ya klabu bingwa Afrika Samatta alivyowapeleka Mazembe fainali ya klabu bingwa Afrika Reviewed by Steve on Monday, October 05, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.