Cheki rekodi aliyofikia John Terry
Nahodha wa Chelsea, John Terry amekuwa mchezaji wa pili wa ndani (mchezaji ambaye sio kipa) kuweza kucheza kila dakika katika kampeni ya timu yake kushinda
Ligi Kuu ya Uingereza.
Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, amekuwa mchezaji wa kwanza wa Chelsea kufanya hivyo tangu Ligi Kuu ilipoanzishwa mwaka 1992.
Mlinzi huyo ambaye ameshatajwa kwenye kikosi bora cha msimu cha Ligi Kuu (PFA Team of The Year) kwa mara ya nne, ‘amemtupia dongo’ (amemdhihaki) kocha wake wa zamani, Rafa Benitez.
Benitez ambaye hakufikisha hata msimu pale Stamford Bridge, alidai mlinzi huyo hawezi kucheza mechi mbili kwa wiki.
Cheki rekodi aliyofikia John Terry
Reviewed by Steve
on
Tuesday, May 26, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, May 26, 2015
Rating:
