Propellerads

Wakala wa Ndemla aweka wazi jinsi Mo alivyokua kikwazo kwa safari ya Sweden



Majeraha ya kiungo wa Simba, Mohamed Ibrahim 'Mo', yametajwa kama chanzo cha kusitishwa kwa muda safari ya Said Ndemla kwenda katika klabu ya AFC Eskilstuna ya Sweden kufanya majaribio.

Akizungumza, Meneja wa Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ambaye alikuwa anafanya mchakato huo, Jamal Kisogo, alisema sababu kubwa iliyofanya Simba kutomruhusu Ndemla ni kutokana na timu hiyo kuandamwa na majeruhi, hasa ya Mo Ibrahim.

Alisema Ndemla alitakiwa kwenda nchini Sweden Februari mwaka huu kwa ajili ya majaribio ambapo alifanya mawasiliano na uongozi wa klabu hiyo na kuambiwa baada ya mechi yao na Majimaji wangemruhusu kwenda, lakini hali ikawa tofauti.

"Baada ya mechi hiyo niliwasiliana na uongozi wa Simba ukanieleza kwamba wanakabiliwa na mechi ngumu na Yanga pia kutokana na majeraha ya Mo Ibrahim wasingeweza kumruhusu kinda wao huyo kwenda kufanya majaribio hayo," alisema.

Pamoja na juhudi hizo, lakini ilishindikana kwa wakati huo, hivyo Kisongo kutoa taarifa kwa AFC Eskilstuna ambao walikubali kusogeza muda huo hadi Machi, lakini imepita na mambo bado hayajakamilika.


Wakala wa Ndemla aweka wazi jinsi Mo alivyokua kikwazo kwa safari ya Sweden Wakala wa Ndemla aweka wazi jinsi Mo alivyokua kikwazo kwa safari ya Sweden Reviewed by Steve on Sunday, April 09, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.