Ulisikia alichokisema Rio Ferdinand juu ya kifo ha mkewe
Kapteni wa zamami wa timu ya taifa ya England Rio Ferdinand ameongea kwa mara ya kwanza hadharani tangu alipompoteza mke wake kwa ugonjwa wa
kansa na kusema kilikua kipindi kigumu kabisa cha maisha yake.
Alimsifia mkewe Rebecca Ellison kama shujaa,na alifariki akiwa na umri wa miaka 34 mwanzoni mwa mwezu huu.
Mlinzi huyo wa QPR pia amesema anajisikia huzuni sana baada ya kukosa michezo kadhaa ya timu yake ambao walikua wakijitahidi kukwepa panga la kushuka daraja.
Mke wake aliemuoa mwaka 2009 alifariki tarehe 1 mei baada ya kuugua muda mrefu kansa ya matiti na ameacha watoto watato ambao ni; Lorenz,{9}, Tate{6} na Tia {4}
Katika maelezo yake Ferdinand amefichua kwamba ugojwa huo wa mkewe ulimfanya alazwe hospitali moja kwa moja ilionekana kwawaida lakini hali ikaja kuwa ngumu sana.
Aliandika “kama mcheza mpira,mara nyingi tumekua tukiongea kuhusu kukosa michezo muhimu kutokana na majeruhi kama vile ndio mwisho wa dunia,
Niamini mimi,sio hivyo kulinganisha na mke wako mama wa watoto wako akifa kwa kansa tena akiwa na umri wa miaka 34 tu.
“Rebecca alikua mwanake hodari ,shujaa na msiri sana ambae hakutaka chochote kuhusu ugojwa wake kuonekana katika vyombo vya habari wakati akipigania maisha yake.ni watu wachache tu wa familia na marafiki wake wa karibu ndi waliojua hilo”.
Alivyoanza kuumwa ilimfanya Ferdinand kuongea na meneja wake kumwondoa kabisa katika majukumu ya timu na alikua hawezi kuchagua upande mwingine zaidi ya kumhudumia mke wake tu.
Aliongeza”nilitaka kuendelea na timu lakini sikua na uhakika kwa kila nitakacho kifanya sikutaka kumpa hofu bosi wangu kama nitakuwepo kwa ajili ya mchezo au sitokuwepo.
“nakubali nilijiskia vibaya sana kwa sababu nilikua naiangusha timu yangu hasa katika mapigano ya kubakia ligi kuu.
“Hakuna hata mmoja aliekua akijua kinachoendelea kwa sababu sikuwaambia,lakini baadae nilimwomba daktari kuwajulisha wachezaji wenzangu”
Tangu kifo wachezaji walitoa pole na rambirambi zao kwa Ferdinand ikiwa pamoja na mshambuliaji Leroy Fer ambae alifunga goli tarehe 2 mei dhidi ya Liverpool na kuonyesha ujumbe wa kuipa pole familia ndani ya fulana aliyoivaa kwa ndani.
Ferdinand aliongeza;” sikuomba ushirikiano mkubwa sana kutoka kwa QPR.kila mmoja alikua karibu na klabu alikua bora sana kwangu.
“siku niliyotangaza Rebecca katutoka nilipata ujumbe mwingi sana kutoka kwa mashabiki.
“kusikia kutoka kwa mashabiki pale Old Trafford na West Ham wakiimba kwa ajili yetu na Steven Gerrard akimkabizi maua mchezaji mwenzangu Joey Barton kilikuwa kitu spesho sana”
Ulisikia alichokisema Rio Ferdinand juu ya kifo ha mkewe
Reviewed by Steve
on
Monday, May 25, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, May 25, 2015
Rating:

