Cesc Fabregas: Sitaacha kuipenda Arsenal
Kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas amedai kua chuki za mashabiki kamwe hazitomfanya
asiipende klabu yake ya zamani ya Arsenal.
Mhispania huyo alijiunga The Gunners akiwa na miaka 16 akiichezea misimu nane kabla ya kwenda Barcelona.
Hata hivyo nyota huyo amekumbana na chuki za mashabiki wa Arsenal na hiki kitu kinatarajiwa kutokea Jumapili ambapo Chelsea na Arsenal wataumana Wembley.
Daily Mail wamemnukuu mkali huyo akisema "Vyovyote vile, mapenzi niliyonayo kwa ile klabu hayatapotea hata ikiwa vipi, nachozingatia ni nini nincho kutoka zamani"
"Mengine sio tatizo, nina kumbukumbu kubwa, mapenzi na heshima kwa klabu. Hutasikia chochote kibaya kutoka kwangu dhidi yao."
Fabregas alipata kuichezea Arsenal mechi 303.
Cesc Fabregas: Sitaacha kuipenda Arsenal
Reviewed by Steve
on
Wednesday, July 29, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, July 29, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment