Propellerads

Mgosi atua Simba kwa mara nyingine tena.

Simba imetangaza kumsajili kwa mara nyingine mshambuliaji wake wa zamani, Mussa Hassan Mgosi.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili ya Simba, Zachakaria Hans Poppe amekubali kwamba Mgosi wamekubaliana kwa mwaka mmoja.

“Tumeshamalizana na Mgosi, tumemrudisha kundini. Kweli tumeridhishwa na kazi yake kwa msimu uliopita.

“Lengo ni kuwa na wakongwe ambao watasaidiana na vijana, tunataka kufanya naye kazi kwa mwaka mmoja,” alisema.
Hata hivyo, Mgosi alisema kwamba hadi Jumatatu, ndiyo atakuwa amemaliza na Simba.


“Kweli ni hivyo lakini hadi Jumatatu tunaweza tukawa tumemmalizana na Simba, nitakueleza vizuri ikiwa tayari,” alisema Mgosi.
Mgosi atua Simba kwa mara nyingine tena. Mgosi atua Simba kwa mara nyingine tena. Reviewed by Steve on Friday, May 29, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.