Propellerads

Kina Msuva, Ngoma walivyoua leo Taifa.



Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara klabu ya Yanga, leo imefanikiwa kuibuka na  ushindi mnono baada ya
kuitandika timu ya Polisi Kombaini kwa magoli 3-0 kwenye mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jioni ya leo
Magoli ya Yanga yamefungwa na Simon Msuva dakika ya 28, Amis Tambwe dakika ya 33 na mshambuliaji mpya wa klabu hiyo aliyesajiliwa kutoka klabu ya FC Platinum ya Zimbabwe Donald Ngoma ambaye amepigilia msumari wa mwisho dakika ya 75 na kuipa timu yake ushindi huo maridhawa.

Mchezo huo ni moja ya maandalizi kwa klabu ya Yanga kuelekea kwenye michuano ya Kagame inayotarajia kuanza kutimua vumbi Agosti 18 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kikosi hicho cha wanajangwani kinatarajia kuingia kambini kesho (Jumatatu) kwa ajili ya kuendelea kujifua kujiandaa na mashindano hayo ya Kagame yanayoshirikisha vilabu bingwa vya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati
Kina Msuva, Ngoma walivyoua leo Taifa. Kina Msuva, Ngoma walivyoua leo Taifa. Reviewed by Steve on Sunday, July 12, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.