Mjue mshambuliaji wa Mbeya City anayewindwa na Simba pamoja na Yanga
Mshambuliaji wa Mbeya City ya jijini Mbeya, Ditram Nchimbi, ameanza kuwindwa na timu mbalimbali za Ligi Kuu Tanzania Bara, zikiwamo Simba na Yanga, kwa ajili ya msimu ujao wa ligi hiyo yenye timu 16.
Nchimbi ameweka wazi kuwa bado ana mkataba na Mbeya City, lakini ameanza kupokea ofa kutoka kwa timu mbalimbali za Ligi Kuu Tanzania Bara, japo yeye hajafanya maamuzi ya kuondoka jijini Mbeya.
"Nashukuru Mungu hivi sasa nipo kwenye hatua nzuri, nimekuwa nikipata ofa mbalimbali kutoka za Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini pia kutoka nje ya nchi, hivyo timu inayotaka kunisajili ifanye mazungumzo na Mbeya City kisha waje kwangu tumalizane," alisema.
Taarifa za awali zinaonyesha kwamba, miongoni mwa timu hizo ni Simba na Yanga, ingawa mwenyewe alipoulizwa ameshindwa kukubali au kukanusha juu ya taarifa hizo.
Mjue mshambuliaji wa Mbeya City anayewindwa na Simba pamoja na Yanga
Reviewed by Steve
on
Sunday, April 09, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment