Propellerads

Mbaraka Yusuf kufuata nyayo za Mbwana Samatta!? vijue vilabu viwili vikubwa Afrika vilivyoanza kumfanyia 'scouting'!!




Baada ya straika wa Kagera Sugar, Mbaraka Yusuf, kuonyesha kiwango kizuri na kusaidia timu yake kupanda hadi nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, tayari baadhi ya klabu kutoka nje ya nchi ikiwemo TP Mazembe ya DR Congo na Etoile du Sahel ya Tunisia zimeanza kummezea mate.

Taarifa za uhakika zilizopatikana kutoka kwa rafiki wa karibu wa mchezaji huyo zinadai kwamba tayari mawakala kutoka nchi hizo mbili wameanza kumfuatilia baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika mechi ya timu ya Taifa, Taifa Stars dhidi ya Burundi.

"Mazembe eako katika skauti ya kusaka wachezaji, wameanza na Tanzania na taarifa zilizopo ni kwamba wamevutiwa sana na kiwango cha Mbaraka (Yusuf) na kuna kila dalili akapata shavu.

"Pia haitakua ajabu akaenda kucheza nchini Tunisia kwani klabu ya Etoile du Sahel, nayo imeonyesha nia ya kuitaka huduma yake.

"Timu hizo zimeanza kuifuatilia Tanzania kwa karibu kutokana na uwezo unaoonyeshwa na straika anayekipiga katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta," alisema rafiki huyo.

Mbaraka mwenyewe alipotafutwa alikiri kuwepo kwa taarifa hizo za kutakiwa na klabu ndani na nje ya nchi lakini akaweka wazi kuwa kwa sasa akili yake ipo katika kuisaidia timu yake kumaliza salama ligi.

"Taarifa za mimi kutakiwa na timu mbalimbali ni za kweli lakini kwa sasa siwezi kusema lolote kwani akili yangu inalenga kuisaidia timu yangu kumaliza salama ligi," alisema.
Mbaraka Yusuf kufuata nyayo za Mbwana Samatta!? vijue vilabu viwili vikubwa Afrika vilivyoanza kumfanyia 'scouting'!! Mbaraka Yusuf kufuata nyayo za Mbwana Samatta!? vijue vilabu viwili vikubwa Afrika vilivyoanza kumfanyia 'scouting'!! Reviewed by Steve on Sunday, April 09, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.