Propellerads

Yanga wamemkamia mkali wa APR...ni noma sana




Yanga imesema inapambana kuhakikisha inamsajili kiungo mkabaji wa
APR, Yannick Mukunzi ili kujiimarisha katika michuano ya kimataifa msimu ujao.

Mukunzi anayevaa jezi namba sita, anafanya vizuri kwenye kikosi cha cha APR inayomilikiwa na Jeshi la Rwanda ambapo sasa viongozi wanafanya kila linalowezekana kuhakikisha inamsajili kiungo huyo.

Mmoja wa mabosi wa Yanga anayeshughulikia usajili, aliliambia Championi Jumamosi kuwa, Mukunzi anaweza kusajiliwa ili kuchukua nafasi ya Mbuyu Twite kutokana na gharama za kuwa naye kuwa kubwa.

“Tunataka kumsajili Mukunzi ili atusaidie katikati kwani tumeona kuna tatizo katika kiungo mkabaji na hata Twite anatumika ndivyo sivyo.
“Hata gharama za kuwa na Twite ni kubwa mno kwani kila mwaka tunapaswa kuilipa FC Lupopo dola 10,000 (Sh milioni 20) kama mkataba unavyosema, kwa hiyo kama tukifanikiwa kumsajili Mukuzi atachukua nafasi ya Twite ikishindikana basi,” alisema bosi huyo.

Hata hivyo awali kumekuwa na taarifa kwamba,  Yanga inasaka beki kutoka katika Kombe la Kagame ili aongeze nguvu katika michuano ya kimataifa.

Ukiacha Cannavaro na Yondani, mabeki wengine wa kati wa Yanga ni Pato Ngonyani, Rajab Zahir anayetarajiwa kutolewa kwa mkopo na kiraka Mbuyu Twite.


Wakati huohuo, straika wa Kpah Sherman anatarajiwa kuondoka kesho Jumapili kwenda Afrika Kusini kufanya vipimo katika Klabu ya Mpumalanga Black Aces ili aweze kujiunga nayo.
Yanga wamemkamia mkali wa APR...ni noma sana Yanga wamemkamia mkali wa APR...ni noma sana Reviewed by Steve on Saturday, July 25, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.