Mkwasa anawahitaji wana Simba
Mashabiki wa Simba, wameitwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kesho kwenda
kuishangilia Yanga ikipambana nan a Al Kharthoum.
Aliyetoa kauli hiyo ni Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa ambaye pia ni kocha wa Taifa Stars.
“Yanga sasa inapambana kuiwakilisha Tanzania, hivyo hata mashabiki wa Simba wanaweza kuwa wazalendo.
“Waje tu, tuungane kwa ajili ya utaifa. Ushabiki wa nyumbani ni baadaye baada ya michuano ya Kagane,” alisema Mkwasa.
Yanga ilianza michuano hiyo kwa kusuasua ikichpwa mabao 2-1 ana Gor Mahia. Lakini ikajirekebisha na kushinda mechi mbili zilizofuata.
Mkwasa anawahitaji wana Simba
Reviewed by Steve
on
Sunday, July 26, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, July 26, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment