Propellerads

Namna mashabiki wa klabu ya Yanga watakavyoweza kuichangia klabu yao



Yanga wajanja sana asikuambia mtu kwani baada ya kugundua kuwa hali yao ya kiuchumi inakwenda mrama, wameamua kuzindua rasmi harambee itakayowajumuisha mashabiki wao kwa ajili ya kuichangia timu kutunisha mfuko wao.

Wanajangwani hao wameingia mkataba na Selcom ambayo watasaidiana kuhakikisha zoezi hilo ambalo limezinduliwa rasmi jana, linakwenda vizuri. Yanga, ambao wako katika hali tete ya kifedha, wameingia mkataba wa miezi miwili na kampuni hiyo kupitia mitandao mitatu ya simu ya Tigo, Vodacom pamoja na Airtel.

Akizungumza  jana Makao Makuu ya Klabu hiyo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Charles Mkwasa, alisema mkakati wao wa harambee walikuwa nao toka mwanzo na sasa wanatimiza tu kile walichokuwa wamekiwaza.

"Hali ya uchumi imeyumba sana kwa kila sehemu, hivyo nina imani Harambee hii inaweza kutusaidia kupata fedha ambazo zitasaidia timu yetu.

"Tumeingia mkataba wa miezi miwili na Kampuni ya Selcom, ambao tutakuwa nao bega kwa bega kuhakikisha zoezi hili linakwenda vizuri na ninaamini tutafanikiwa," alisema.

Akizungumzia madeni katika klabu yao, alisema mpaka sasa hawadaiwi na Kampuni yoyote, isipokuwa madeni waliyonayo ni mishahara ya wachezaji na kusema kwamba wanafanya kila linalowezekana kutatua tatizo hilo.
Namna mashabiki wa klabu ya Yanga watakavyoweza kuichangia klabu yao Namna mashabiki wa klabu ya Yanga watakavyoweza kuichangia klabu yao Reviewed by Steve on Tuesday, April 25, 2017 Rating: 5

1 comment:

Anonymous said...

The Best Casino Sites in India 2021 - ChoegoCasino
Read 제왕 카지노 about the top casinos in India 2021, and get a list of the top casino sites you 인카지노 can 카지노 play with bonuses.

Propellerads
Powered by Blogger.