Kuelekea mchezo na Azam, Simba waamua kujichimbia Moro
Simba wanajua kuwa wanakabiliwa na mchezo mgumu wa Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Azam FC, na sasa wameamua kulisusa jiji la Dar es Salaam na kukimbilia mkoani Morogoro kujichimbia kwa muda kuwawinda Wanalambalamba hao.
Wekundu hao wa Msimbazi walitua Morogoro jana jioni kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao huo wa nusu fainali ya FA, utakaopigwa Jumamosi ya wiki hii Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Wekundu hao wa Msimbazi wameamua kwenda kuweka kambi yao mji kasoro bahari, ikiwa ni baada ya jana asubuhi kufanya mazoezi yao katika uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini, jijini Dar es Salaam.
Wakiwa Morogoro, Simba watajichimbia katika hosteli za Kanisa la Baptist zilizopo katika milima ya Uluguru kuendelea na maandalizi ya pambao hilo la kukata na shoka.
Meneja wa timu hiyo, Mussa Hassan Mgosi amesema timu hiyo imeondoka jana jioni kwenda Mji kasoro Bahari kuweka kambi yake na kuahidi kufanya makubwa zaidi kwenye mchezo huo.
Mgosi lisema wachezaji wote wa kikosi hicho wapo vizuri, isipokuwa na Method Mwanjali, ambaye bado ni majeruhi na hakuambatana na timu hiyo, kwni bado anaendelea na matibabu.
"Azam ni timu nzuri, tunaiheshimu, hivyo tunakwenda kujipanga kuhakikisha tunapata ushindi n kuingia fainali katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali, kwani kila timu inatafuta nafasi," alisema.
Simba itacheza na Azam, Jumamosi ya wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, wakati Yanga watalazimika kusafiri kwenda mkoani Mwanza kukutana na Mbao kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, mchezo utakaochezwa Jumapili ya wiki hii.
Kuelekea mchezo na Azam, Simba waamua kujichimbia Moro
Reviewed by Steve
on
Tuesday, April 25, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment