Propellerads

Simba waamua kumuweka kando Mwanjali kwa msimu huu



Baada ya beki wa Simba Mzimbabwe, Method Mwanjale kuka nje ya dimba kwa takribani miezi miwili sasa akiuguza majeraha ya goti, hatimaye benchi la ufundi la timu hiyo limeamua kumuondoa rasmi kwenye mipango yao katika mechi zao za kumaliza msimu huu.

Mwanjale ambaye aliumia Februari 11, mwaka huu kwenye mchezo dhidi ya Prisons ambao Simba waliibuka na ushindi wa mabao 3-0, tangu siku hiyo hakuweza kuitumikia tena timu hiyo mpaka leo akiwa anaendelea kupata matibabu ya majeraha yake.

Jackson Mayanja ambaye ni kocha msaidizi wa kikosi hicho, amesema:

"Huyo kwa sasa usimuhesabie kwanza kwani bado anapatiwa matibabu na hata kama akipona sasa hivi hawezi kucheza kwa sababu hatakuwa fiti.

"Kwa kitendo chake cha kukaa nje miezi miwili bila ya kucheza, kitaalamu na kiufundi itakuwa ni vigumu kucheza kwa sasa kwani ukiangalia mechi zilizosalia si za kujaribu wachezaji, hivyo Mwanjale kwa sasa hatumuhesabii."
Simba waamua kumuweka kando Mwanjali kwa msimu huu Simba waamua kumuweka kando Mwanjali kwa msimu huu Reviewed by Steve on Wednesday, April 26, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.