Azam wanamtaka Haji Mwinyi wa Yanga, mwenyewe aweka wazi mchongo mzima ulivyokaa
Beki wa kushoto wa Yanga, Haji Mwinyi ameingia katika rada za timu ya Azam ambayo inadaiwa kuwa katika harakati za kuitafuta saini yake ili aweze kuitumikia katika msimu ujao wa Lig Kuu Bara.
Azam inadaiwa kufikia uamuzi huo baada ya kupata taarifa kuwa mkataba wa beki huyo na Yanga unafikia tamati hivi karibuni lakini pia uongozi wa timu hiyo unataka kumpatia Sh milioni 20 ili aweze kuongeza mkataba.
Habari za kuaminika ambazozimepatikana zinadai kwamba Yanga imemtaka mchezaji huyo achukue fedha hizo lakini yeye anataka apewe zaidi kwani thamani yake ya sasa siyo ya Sh milioni 20.
"Kwa hiyo Azam baada ya kusikia hivyo wameanza mikakati ya kumuwania beki huyo na hivi karibuni baadhi ya viongozi wa timu hiyo walikutana naye," kilisema chanzo cha habari.
Alipoulizwa kuhusiana na suala hilo, Mwinyi alisema: "ni kweli kabisa mkataba wangu na Yanga unamalizika hivi karibuni na nimeshafanya mazungumzo na uongozi wangu wa Yanga kwa ajili ya mkataba mpya lakini hatujafikia makubaliano kuhusiana na dau wanalotaka kunipatia.
"Kuhusiana na Azam, ni kweli wamenifuata lakini kwa sasa nawasikiliza kwanza Yanga ambao ndiyo walionifanya niwe hapa nilipo, kama hatutafikia makubaliano ndipo nitaamua nini cha kufanya, kama ni kwenda Azam au sehemu nyingine," alisema Mwinyi.
Azam wanamtaka Haji Mwinyi wa Yanga, mwenyewe aweka wazi mchongo mzima ulivyokaa
Reviewed by Steve
on
Wednesday, April 26, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment