Mbao FC wajitapa kuzijua siri za kuwamaliza Yanga Jumapili
Mbao FC wamedai wamenasa mipango ya siri ya Yanga, ikiwa ni siku chache kabla ya kucheza mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (FA), itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.
Akizungumza jana, Makamu Mwenyekiti wa Mbao, Erick Gosso, alidai wamefanikiwa kupata siri nyingi zilizowawezesha Yanga kushinda katika michezo yao iliyopita.
Gosso alidai itakuwa ni rahisi kwao kushinda katika mechi hiyo, kwani wamejua mbinu wanazotumia Yanga kushinda mechi zao.
Alidai wao wamejizatiti kushinda na kuiondoa Yanga katika michuano hiyo ili waweze kucheza fainali. Gosso alisema hawana wasiwasi kwa kuwa wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi, hasa baada ya kunasa mipango yao ya siri inayowawezesha kushinda.
"Ukijua siri za mpinzani wako ni rahisi kummaliza na hivyo ndivyo ilivyo kwetu, kila kitu cha Yanga kipo katika mikono yetu, wakija wajiandae kupata maumivu," alisema Gosso.
Mbao FC wajitapa kuzijua siri za kuwamaliza Yanga Jumapili
Reviewed by Steve
on
Thursday, April 27, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment