Propellerads

Kina Msuva walivyokinukisha leo na Yanga, jua yote hapa pamoja na picha baadhi


Yanga kulitetea Kombe inalolishikilia la Ligi Kuu bara kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya
Coastal Union.
Kwa ushindi huo wa mabao mawili na kupata pointi tatu, Yanga inayonolewa na Mholanzi, Hans van der Pluijm inakaa kileleni mwa Ligi Kuu Bara.


Yanga imepata ushindi huo leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku mabao yote yakifungwa katika kipindi cha kwanza.
Simon Happygod Msuva na Donald Ngoma raia wa Zimbabwe ndiyo waliofunga mabao hayo mawili ya Yanga.


Ahmed Shiboli wa Coastal Union alipoteza nafasi tatu safi za kufunga ambazo zingewasaidia angalau kupata bao la kufutia machozi au kusawazisha zaidi.
Yanga bao walipoteza nafasi nyingine tatu kupitia Amissi Tambwe, Msuva na Haruna Niyonzima.
Yanga ambao ni mabingwa watetezi wanaungana na Simba, Toto African, Majimaji, Azam FC, Mtibwa Sugar na Kagera Sugar kuwa timu zilizoanza na ushindi katika siku ya kwanza ya ligi.
Leo kulikuwa na mechi hiyo moja kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union wakati pazia la ligi hiyo lilifunguliwa jana kwa mechi saba kuchezwa.










Ungana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na tuffollow Twitter @Kandanda 24

Kina Msuva walivyokinukisha leo na Yanga, jua yote hapa pamoja na picha baadhi Kina Msuva walivyokinukisha leo na Yanga, jua yote hapa pamoja na picha baadhi Reviewed by Steve on Sunday, September 13, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.