Kuelekea mchezo bwa Arsenal, Ivanovic anataka hiki kwa timu yake
Nyota wa Chelsea, Branislav Ivanovic amewataka wachezaji wenzake kua ni lazima
wapate ushindi jumamosi ijayo dhidi ya Arsenal.
Mabingwa hao watetezi wamejikuta wakipoteza mchezo wa tatu kati ya michezo mitano waliyocheza msimu huu baada ya kufungwa kwa 3-1 dhidi ya Everton juzi jumamosi.
Kwa sasa The Blues wako nafasi ya 11 kwenye msimamo, kuhusu mechi inayofata na Arsenal, Ivanovic amewataka wenzie kwa sasa kullenga katika kushinda michezo tu na sio kushindana na vilabu vingine kwanza.
"Bila shaka Arsenal wako vizuri. Kawaida hua ni ngumu sana dhidi ya Arsenal, lakini tunatakiwa tujiangalie sisi wenyewe" aliongea kama alivyonukuliwa na The Mirror.
"Tunatakiwa tuamini kitu kimoja- mchezo ujao. Hatuwezi kuanza kuzifikia timu nyingine ila ni kushinda mchezo kwa mchezo. Hatutakiwi kufikiria kitu kingine zaidi."
The Gunners katika mchezo wao mwisho waliwafunga Chelsea 1-0 na kuchukua ngao ya jamii, na katika mchezo huo Wenger ndipo aliupofuta uteja wa muda mrefu wa kufungwa na Mourinho.
Ungana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na tuffollow Twitter @Kandanda 24
Kuelekea mchezo bwa Arsenal, Ivanovic anataka hiki kwa timu yake
Reviewed by Steve
on
Monday, September 14, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, September 14, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment