Propellerads

Mavugo atamba kuendeleza dozi hata mbele ya Kagera Sugar



Mshambuliaji wa Simba, Laudit Mavugo, ametamba kuendeleza makali yake ya kuzifumania nyavu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar.

Mavugo amesema amejipanga vizuri kwa ajili ya mechi hiyo na atahakikisha anapambana ili waweze kuibuka na ushindi.

Mbali na hilo, Mavugo mwenye mabao saba katika ligi hiyo, amesema amejipanga pia kuhakikisha anaiendeleza rekodi yake ya kuzifumania nyavu mfululizo ambayo amewika nayo hivi karibuni kwa kufunga mfululizo tangu alipotoka kwenye balaa la kucheza kwa muda mrefu bila ya kufunga.

"Tunaendelea na mandalizi yetu vizuri na tumejipanga ili kuhakikisha tunapata ushindi katika mechi hiyo lakini pia binafsi nimejiandaa kuiendeleza rekodi yangu ya kufunga mfululizo ambayo nimeiweka hivi karibuni baada ya kupitia kwenye wakati mgumu hapo nyuma.

"Kagera Sugar ni timu nzuri, tunaiheshimu lakini ni lazima tuifunge ili tuweze kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa ambao ndiyo lengo letu kubwa msimu huu," alisema Mavugo.


Mavugo atamba kuendeleza dozi hata mbele ya Kagera Sugar Mavugo atamba kuendeleza dozi hata mbele ya Kagera Sugar Reviewed by Steve on Friday, March 31, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.