Kuelekea mchezo na Kagera Sugar, Ajibu atoa wasiwasi mashabiki wa Simba kuhusu maumivu aliyoyapata mechi ya Stars na Burundi
Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu, amefunguka kwa kusema kuwa nia yake ni kujituma kwa nguvu zote kuisaidia timu yake kuchukua ubingwa lakini kuelekea mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar napo ametoa neno.
Kuonyesha kuwa yupo tayari kwa lolote, Ajibu ambaye alipata maumivu alipokuwa akiitumikia Taifa Stars dhidi ya Burundi Jumanne ya wiki hii na hivyo kumalizika kutoka moja kwa moja uwanjani, amesema yupo tayari kucheza mchezo dhidi ya Kagera hata kama atakuwa na maumivu.
"Kweli nina maumivu lakini kwa kizungu tunaita ni 'small pain' hivyo hayawezi kunizuia mimi kucheza dhidi ya Kagera, naamini ndani ya siku mbili tatu nitakuwa vyema na maumivu yatakata na kuweza kuendelea na mchakato wa kusaka ubingwa.
"Tunahitaji kushinda katika michezo yetu yote iliyo mbele yetu kwani tunajituma ipasavyo kuweza kufanikiwa kufanya vyema kwani kila mchezo tutakaocheza utakuwa na ushindani mkubwa, hivyo siyo muda wa kupoteza nafasi."
Kuelekea mchezo na Kagera Sugar, Ajibu atoa wasiwasi mashabiki wa Simba kuhusu maumivu aliyoyapata mechi ya Stars na Burundi
Reviewed by Steve
on
Friday, March 31, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment