Unamkumbuka Mbuyu Twite!!?, huu hapa ujumbe mahsusi amewapa Wanayanga
Kiungo wa zamani wa Yanga, Mnyarwanda, Mbuyu Twite, ameibuka na kudai kuwa katika mechi sita zilizosalia za Ligi kuu Bara lolote linaweza kutokea na si kuanza kutabiri ubingwa kwa sasa.
Twite ambaye kwa sasa anakipiga kwenye kikosi cha Fanja FC ya Oman, amejiunga na timu hiyo mwishoni mwa mwaka jana baada ya mkataba wake na Yanga kumalizika katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo msimu huu.
"Nipo huku lakini naifuatilia ligi ya Tanzania kupitia mitandao mbalimbali, najua Simba wanaongoza wakifuatiwa na Yanga, japo bado mechi zimesalia chache ligi imalizike, lakini naamini lolote linaweza kutokea kati ya timu hizi mbili na si kusema sasa aliye juu anaweza kuwa bingwa kwani anaweza kushushwa na kumaliza akiwa wa pili.
"Tangu nifike huku, nimekutana na ugumu ambao sikutarajia, nina siku chache huku lakini tayari nimeona tofauti kubwa ya ligi ya Tanzania na ya Oman, lakini kitu kizuri ni kwamba nimeweza kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza japo ugumu wake ni sawa na Tanzania," alisema Twite.
Unamkumbuka Mbuyu Twite!!?, huu hapa ujumbe mahsusi amewapa Wanayanga
Reviewed by Steve
on
Friday, March 31, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment