Kukosekana kwa Mwanjali imekua pengo kwa Msimbazi, hii hapa michezo waliyopoteza bila uwepo wake
Beki wa kati wa Simba, Method Mwanjali amedhihirisha umuhimu wake ndani ya timu hiyo baada ya kubainika amekuwa akiigharimu kila anapokosekana dimbani.
Mwanjali yupo nje ya uwanja akiuguza majeraha baada ya kuumia wakati wa mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Prisons iliyochezwa Februari 11.
Katika michezo mitano ambayo beki huyo alikosekana uwanjani, Simba imeshinda michezo miwili ambao ni ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Yanga na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mbao FC.
Pili ililazimishwa sare ya 2-2 na Mbeya City na suluhu ya 0-0 dhidi ya Toto Africans, huku ikipoteza mchezo mmoja kwa kuchapwa mabao 2-1 na Kagera Sugar.
Pia katika michezo hiyo, safu ya ulinzi ya Simba iliruhusu wavu wao kuguswa mara tano mwenendo ambao haukuonekana katika mechi ambazo Mwanjali alikuwemo kikosini.
Kukosekana kwa Mwanjali imekua pengo kwa Msimbazi, hii hapa michezo waliyopoteza bila uwepo wake
Reviewed by Steve
on
Tuesday, April 18, 2017
Rating:
1 comment:
Yah ni hiyo ni nzuri kwasababu uwezo wa yanga kuchukua kombe bado uko na hakuna umuhimu wa kuzungumzia sakata la fakki Mohammed ukiangalia mechi walizobakia Nazo ni tano na ikotokea wameshinda zote watakuwa wamechukua kombe mfululizo.
Post a Comment