Propellerads

Kuhusu mjadala wa kadi tatu za Fakhi, uongozi Yanga waamua kuwapiga marufuku wachezaji wake




Uongozi wa Yanga kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake, Clement Sanga, umewapiga 'stop' wachezaji wa timu hiyo kuzungumzia masuala ya kadi tatu za njano yanayomhusu beki wa Kagera Sugar, Mohamed Fakhi.

Uongozi wa Yanga wenyewe umesema kuwa hautaki kuwaona wachezaji wao wakijadili kuhusu kadi hizo bali waendelee kupambana uwanjani kwani wakishinda michezo yao yote bado wanaweza kua mabingwa.

Sanga amesema kuwa haoni sababu ya Msuva au mchezaji yeyote wa Yanga kwa kipindi hiki kujadili mambo ya Simba na Kagera Sugar wakati mambo hayo si ya Yanga bali ni ya kamati za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na walalamikaji husika.

"Kweli kwa sisi tusingependa sana kwa kipindi hiki kumuona mcezaji yeyote wa Yanga akitumia muda wake mwingi kuwazia mambo ya kadi tatu za Fakhi au kuanza kujadili suala hilo.

"Maana tungependa kuelekeza mawazo na akili zetu katika michezo iliyosalia, kwani matokeo yanaweza kupatikana uwanjani tu na siyo sehemu nyingine," alisema Sanga.
Kuhusu mjadala wa kadi tatu za Fakhi, uongozi Yanga waamua kuwapiga marufuku wachezaji wake Kuhusu mjadala wa kadi tatu za Fakhi, uongozi Yanga waamua kuwapiga marufuku wachezaji wake Reviewed by Steve on Wednesday, April 19, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.