Propellerads

Safari ya Banda kuelekea Sauzi, mambo yapo namna hii...



Kiza kimetanda kuhusu safari ya beki wa Simba, Abdi Banda nchini Afrika Kusini kufanya majaribio baada ya wahusika kutokuwa wazi.

Banda ambaye alisimamishwa kucheza Ligi Kuu na Kamati ya Uendeshaji wa Ligi 'Kamati ya Saa 72' kwa kosa la kumpiga ngumi mkongwe, George Kavila, inasemekana anatakiwa na klabu ya Kaizer Chief ya nchini humo lakini mpaka sasa undani wa safari yake umekuwa kitendawili kilichokosa jibu.

Taarifa za awali ambazo zilithibitishwa na Banda mwenyewe, zilidai kuwa beki huyo angeondoka nchini Jumatano iliyopita kuelekea Afrika Kusini, lakini inaaminika kuwa mpaka sasa yupo jijini Dar es Salaam akila maisha.

Rais wa Simba, Evans Aveva alipotafutwa kuhusu kutolea ufafanuzi ishu hii nae alijibu kwa kifupi kwa kusema beki huyo haendi popote.

"Bandayupo nchini hajaenda popote sisi hizo taarifa za kutakiwa Afrika Kusini hatujazisikia na kama zipo kwetu hazijafika rasmi," alisema Aveva.

Kwa upande wake meneja wa zamani wa mchezaji huyo, Abdul Bosnia alipoulizwa kuhusiana na safari ya Banda alisema kwa wakati huo hakuwa na jipya lakini akaahidi kueleza kila kitu pale mpango huo utakapokua umekamilika. "Mimi nimetoka Tanga nipo Dar kushughulikia masuala yake, siwezi kuzungumza kila kitu wakati mambo bado hayajakamilika lakini tukishafikia mwafaka tutaweka wazi kila kitu," alisema Bosnia.
Safari ya Banda kuelekea Sauzi, mambo yapo namna hii... Safari ya Banda kuelekea Sauzi, mambo yapo namna hii... Reviewed by Steve on Tuesday, April 18, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.