Abramovich kumzuia Hazard kuondoka, Mourinho ampiga 'beat' Pogba.....stori za usajili kutoka magazeti ya Ulaya leo Ijumaa
Eden Hazard hataondoka klabuni Chelsea majira haya ya joto, hii ni kwa mujibu wa gazeti la Daily Express.
Real Madrid walihusishwa na kutaka kumsajili Mbelgiji huyo lakini hata hivyo tajiri wa timu, Abramovich hataki kumwachia nyota huyo wa zamani wa Lille.
The Express linadai kwamba Abramovich atazuia juhudi zozote za Real Madrid kumsajili hata kama kocha Antonio Conte atakua tayari kumuuza.
Hizi hapa ni 'Top stories' kutoka magazeti ya leo Ijumaa.
- Chelsea wana imani kubwa kwamba watawazidi kete katika harakati za kumsajili beki Mholanzi wa Southampton, Virgil van Dijk kwa dau la pauni mil 50.
- Yohan Cabaye yupo katika mipango ya kuondoka Crystal Palace na kutimkia Marseille ya Ufaransa.
- Vilabu vinne vya Premier League vipo katika vita vya kumuwinda beki w Dynamo Kiev, Domagoj Vida, vilabu hivyo ni West Ham, Stoke, Everton na Sunderland.
- Jose Mourinho 'amemcha' Paul Pogba kupunguza kuendekeza mambo mengi ya kibiashara nje ya uwanja na badala yake kuelekeza nguvu zake uwanjani.
Abramovich kumzuia Hazard kuondoka, Mourinho ampiga 'beat' Pogba.....stori za usajili kutoka magazeti ya Ulaya leo Ijumaa
Reviewed by Steve
on
Friday, March 31, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment