Aliyefunga bao la Stars dhidi ya Burundi amewapa salamu hizi Msimbazi kulekea mchezo na Kagera Sugar.
Mshambuliaji wa Kagera Sugar, Mbaraka Yusuph, amesema bao aliloifungia timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' dhidi ya Burundi ni salamu tosha kwa wapinzani wao Simba watakapokutana nao Jumapili.
Mbaraka amesema Simba wasitaajie mteremko kwenye mchezo huo kwani na wao wamejipanga vema kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo huo.
"Lile bao ni salamu tosha kwa mashabiki wa Simba, hata wachezaji wao wajue Jumapili hakuna mteremko kwa kuwa kila timu inahitaji ushindi kuelekea mchezo huo," alisema mshambuliaji huyo ambaye kabla ya kutua Kagera Sugar alikua katika kikosi cha vijana cha Simba 'Simba B'
Aliyefunga bao la Stars dhidi ya Burundi amewapa salamu hizi Msimbazi kulekea mchezo na Kagera Sugar.
Reviewed by Steve
on
Thursday, March 30, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment