Man United wamtengea dau la kutosha Lukaku, Sanchez atoa masharti ya kuendelea kukaa Arsenal....hizi hapa stori za Usajili magazeti ya Ulaya Alhamisi hii
Klabu ya Manchester United ipo tayari kufanya usajili mkubwa majira ya kiangazi kwa kumnasa nyota wa Everton, Romelu Lukaku kwa dau la pauni mil 70.
Kocha Jose Mourinho amekua na wakati mgumu kuhusu swala la washambuliaji kikosini kwake msimu huu kutokana na washambuliaji tegemezi kusumbuliwa na majeraha na wengine kutokua katika viwango vyao.
Huku pia Zlatan Ibrahimovic akionekana kua tayari kuendelea kukaa na klabu hiyo msimu ujao, lakini kocha huyo Mreno anaonekana kuhitaji nguvu zaidi kujiimarisha.
Hizi hapa habari nyingine kutoka magazeti ya leo Alhamisi
- Alexis Sanchez amedokeza kwamba ataendelea kukaa Arsenal endapo tu ataona kuna hali ya ushindi, mkataba wake wa sasa unaelekea ukingoni ambapo kuna hofu endapo atongeza tena.
- Liverpool nao katika kinyang'anyiro cha kunasa huduma ya Dele Alli.
- Manchester United bado wanafanya juhudi za kuipata saini ya kiungo wa Monaco, Tiemoue Bakayoko kwa pauni mil 40 ambaye pia Chelsea wanamfukuzia.
- Beki wa Atletico Madrid, Jose Gimenez yupo tayari kuhamia Man United kiangazi hiki.
- Zlatan Ibrahimovic amedokeza kwamba yupo tayari kuongeza mkataba mwingine tena ndani ya Manchester United.
- Kwa mujibu wa vyanzo kutoka Italia, beki wa Arsenal, Hector Bellerin yupo katika rada za wakali wa Serie A, Juventus.
- Arsenal na Man Utd wanahusishwa na winga wa Villareal anayetajwa kua na thamani ya pauni mil 35, Samuel Castillejo lakini pia wakipata ushindani kutoka Man City na Napoli.
- Liverpool wameonesha kua kuihitaji huduma ya nyota wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain majira ya kiangazi.
Man United wamtengea dau la kutosha Lukaku, Sanchez atoa masharti ya kuendelea kukaa Arsenal....hizi hapa stori za Usajili magazeti ya Ulaya Alhamisi hii
Reviewed by Steve
on
Thursday, March 30, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment