Chelsea wanamtaka Sanchez, Wenger na mipango ya miaka kumi Arsenal.....magazeti ya Ulaya leo yana hizi kuhusu usajili
Chelsea wanataka kuwaleta kikosini Stamford Bridge Alexis Sanchez na Romelu Lukaku majira ya kiangazi, hii ni kwa mujibu wa gazeti la Daily Telegraph.
Sanchez mkataba wake na Arsenal unafikia tamati majira ya kiangazi 2018 kitu ambacho kitawalazimu Gunners kumuuza mwishoni msimu huu ili asije akaondoka bure kama mchezaji huru.
Kwa upande wa Lukaku bado amekua katika kiwango kinachoridhisha tangu aondoke Chelsea mwaka 2014, na sasa wanamuhitaji tena.
Hizi hapa 'Top stories' nyingine kutoka magazeti ya Ulaya kuhusu usajili leo
- Bosi wa Chelsea, Antonio Conte amemwambia Eden Hazard asahau swala la kujiunga na Real Madrid.
- West Ham wanatazamia kufanya usajili wa majira ya kiangazi kwa mshambuliaji wa Arsenal, Lucas Perez.
- Aston Villa wanajipanga kufanya mazungumzo na Manchester United ili kuongeza muda wa Sam Johnstone kuendelea kukaa Midland.
- Bosi wa Arsenal, Arsene Wenger anaweka mipango ya miaka mingine kumi ijayo ndani ya Emirates.
- Bosi wa Bournemouth, Eddie Howe amefunguka kwamba anafikiria kumrejesha Jermaine Defoe.
Chelsea wanamtaka Sanchez, Wenger na mipango ya miaka kumi Arsenal.....magazeti ya Ulaya leo yana hizi kuhusu usajili
Reviewed by Steve
on
Saturday, April 01, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment