Kuelekea mchezo wa Yanga na Azam leo, Niyonzima atoa neno
Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima anaamini kabisa kama timu yake inataka kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara, ni lazima leo Jumamosi iifunge Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Niyonzima ambaye ni raia wa Rwana, amesema mchezo huo utakua mgumu kulingana na historia yao kila wanapokutana lakini kwao ni muhimu kwani wakishinda watakuwa mwanga mzuri wa kutwaa ubingwa.
"Mechi yetu na Azam ni mchezo mkubwa na utakuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na kila upande kuhitaji ushindi, lakini tumejipanga kushinda kwani ndiyo mechi ambayo itatoa mwelekeo wa kutetea ubingwa wetu.
"Ni lazima tushinde mechi hii ili tujiweke katika nafasi ya kutwaa ubingwa kwa mara ya tatu mfululizo, tuna majeruhi wengi lakini tutapambana ili tushinde," alisema Niyonzima.
Kuelekea mchezo wa Yanga na Azam leo, Niyonzima atoa neno
Reviewed by Steve
on
Saturday, April 01, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment