Propellerads

Kuhusu ishu ya nyasi za Simba pale bandarini na TRA, Evans Aveva afunguka hivi




Baada ya juzi Alhamisi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutangaza kuwa inatarajia kuzipiga mnada nyasi bandia za Simba kupitia kwa Kampuni ya Udalali ya Majembe Auction Mart, uongozi wa klabu hiyo hivi sasa unahangaika kuhakikisha unazikomboa kabla ya kufanyika zoezi hilo.

Nyasi hizo ambazo uongozi wa Simba uliziagiza kutoka China kwa ajili ya kuziweka kwenye uwanja wao uliopo Bunju, Dar es Salaam, zina zaidi ya miezi mitano tangu zilipowasili bandarini hapo na uongozi wa klabu hiyo umekuwa ukisuasua kuzilipia ushuru ili uweze kuzichukua.

Kutokana na muda wa nyasi hizo kuwa bandarini hapo kupita bila kulipiwa ushuru , ndipo TRA  ilipoamua kutangaza mnada na sasa Rais wa Simba, Evans Aveva amefungukia ishu hiyo,

"Taarifa hizo tumezipata na hivi sasa tunapambana vilivyo kuhakikisha tunazikomboa.

"Kwa sasa hatuna cha kujitetea kuhusiana na suala hilo ila kilichopo kwetu ni kuhakikisha tunatekeleza agizo hilo la serikali." alisema Aveva.
Kuhusu ishu ya nyasi za Simba pale bandarini na TRA, Evans Aveva afunguka hivi Kuhusu ishu ya nyasi za Simba pale bandarini na TRA, Evans Aveva afunguka hivi Reviewed by Steve on Saturday, April 01, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.