Propellerads

Mkude azungumzia hali ya kikosi kuelekea michezo ya Kanda ya Ziwa.




Jonas Mkude amesema timu yake ya Simba imejipanga kikamilifu kuhakikisha inashinda mechi zote za Kanda ya Ziwa wakianza na Kagera Sugar kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Kaitaba, ili waweze kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bra.

Simba ina mechi tatu Kanda ya Ziwa kati ya sita walizobakiza katika ligi kuu ambapo inaanza kucheza na Kagera Sugar ya Kagera, halafu Mbao FC kisha Toto Africans zote za Mwanza.

Akizungumzia michezo hiyo, Mkude ambaye ni kiungo na nahodha wa Simba amesema kikosi chao kipo vizuri kuhakikisha wanaifunga Kagera Sugar licha ya kuutambua uwezo wa kipa Juma Kaseja wa timu hiyo.

"Tumejpipanga vyema kuona tunafanikiwa kushinda mechi zetu zote za kanda ya Ziwa, kwani kuna ushindani na ugumu wa hali ya juu, hivyo tunahitaji kushinda na kuibuka na kuibuka na pointi tatu katika kila mechi.

"Mechi hizi za mwisho ni ngumu kuna timu ambazo zinawania kutoshuka daraja na nyingine zinawania kutwaa ubingwa na iwapo tutateleza mechi yetu yeyote huku tunaweza kukosa ubingwa.

"Kwa ujumla wachezaji wote wapo vizuri na kila mmoja amejiandaa vyema kukabiliana na Kagera na kisha Mbao halafu Toto na lengo ni ubingwa tu msimu huu, tutajituma hadi dakika za mwisho," alisema Mkude.

Mkude azungumzia hali ya kikosi kuelekea michezo ya Kanda ya Ziwa. Mkude azungumzia hali ya kikosi kuelekea michezo ya Kanda ya Ziwa. Reviewed by Steve on Saturday, April 01, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.