Propellerads

Waarabu wajitapa kuwafahamu vizuri Yanga kupitia Simba, haya ni maneno ya kocha wao




Wapinzani wa Yanga katika Kombe la Shirikisho Afrika, MC Alger wametua nchini juzi usiku halafu jana jioni wakafanya mazoezi na kupiga mkwara mzito wakidai wanawajua vizuri Wanajangwani.

Akizungumza, meneja wa timu hiyo, Nacer Buiche, alisema baada ya ratiba kutolewa haraka walianza kuifuatilia Yanga kwa karibu ili kujua mbinu na aina ya wachezaji walionao.

Buiche aliseama, wameijua zaidi Yanga kupitia Simba ambao wamepata taarifa ndiyo wapinzani wao wakubwa nchini pia kwa kuziangalia video za mechi zao walizozicheza kwa kupitia mitandao.

Alisema wanaiheshimu Yanga lakini wataingia uwanjani kwenye mechi hiyo kwa ajili ya kupata ushindi wa ugenini kabla ya kurudiana nao Algeria.

"Tunaingia uwanjani tukiwa tayari tunawajua wapinzani wetu Yanga, kwani mara baada ya ratiba kutangazwa na sisi kupangwa nao, haraka tukaanza kuifuatilia kwa karibu.

"Niseme kuwa, tunaijua vizuri Yanga ambao wapinzani wao wakubwa hapa nchini ni Simba, hivyo tumebahatika kuziona baadhi ya mechi zao zikiwemo dhidi ya Simba.

"Hivyo basi maandalizi tumeyafanya ya kutosha kuhakikisha tunapata ushindi kwa kuanzia mechi hii ya hapa ugenini hadi ile ya marudiano," alisema Buiche.
Waarabu wajitapa kuwafahamu vizuri Yanga kupitia Simba, haya ni maneno ya kocha wao Waarabu wajitapa kuwafahamu vizuri Yanga kupitia Simba, haya ni maneno ya kocha wao Reviewed by Steve on Saturday, April 08, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.