Huyu hapa Ajibu akiweka wazi juu ya tetesi za kusaini Yanga
Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu amefunguka juu ya kuhusishwa na kujiunga na Yanga katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara akisema hajui lolote kuhusu madai hayo na ataweka wazi kila kitu atakapomaliza mkataba wake.
Licha ya kupewa mkataba mpya na Simba, Ajibu bado hajausaini akisisitiza atafanya jambo hilo baada ya kumalizika kwa ligi ambapo pia mkataba wake na klabu hiyo utakuwa umefikia tamati.
Hivi karibuni kumekuwepo na taarifa za Yanga kumuweka Ajibu katika mipango yao ya msimu ujao huku wakitajwa kuwa chanzo cha mshambuliaji huyo kutosaini mkataba wa Simba.
Kuhusu swala hilo, Ajibu mwenyewe amefunguka: "Mimi sijui chochote juu ya madai ya Yanga kunihitaji nimekua nikisikia tu, na siwezi kusema lolote hadi mkataba wangu utakapoisha.
"Ninachokiangalia hivi sasa ni kuona ni jinsi gani naisaidia timu yangu kwani lengo letu ni kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu kwa kuhakikisha tunashinda mechi zote zilizobakia," alisema Ajibu.
Mkataba wa kiungo huyo mwenye mabao sita kwenye ligi na klabu yake ya Simba unafika ukingoni mara baada ya msimu kumalizika ambapo pia taarifa zinasema anaweza kutimkia Afrika Kusini.
Huyu hapa Ajibu akiweka wazi juu ya tetesi za kusaini Yanga
Reviewed by Steve
on
Saturday, April 08, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment