Ijue programu maalum aliyoandaa kocha Lwandamina kwa ajili ya Waarabu leo
Yanga leo saa 10:00 jioni itacheza mechi ya kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya MC Alger ya Algeria, katika kuhakikisha wanashinda Kocha George Lwandamina amewaandaa wachezaji wake kutumia zaidi mipira ya mbali kupata mabao.
Yanga inacheza mchezo huo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo katika mazoezi yake juzi na jana uwanja huo huo wa Taifa, kocha Lwandamina akiwa na wasaidizi wake, Juma Mwambusi na Noeli Mwandila, waliandaa progranu ya dakika 30 kwa wachezaji wa timu kupiga mashuti makali nje ya 18 huku wakirudia zaidi ya mara tatu.
Akizungumza kuhusu mazoezi hayo, Mwambusi alisema: "Kile tulichokuwa tunakifanya ni sehemu ya programu zetu kwa sababu katika mechi lolote linaweza kutokea, tunataka timu iwe imara."
Ijue programu maalum aliyoandaa kocha Lwandamina kwa ajili ya Waarabu leo
Reviewed by Steve
on
Saturday, April 08, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment