Real Madrid wamng'ang'ania Isco,, pia kuwasajili Hazard, De Gea.....tetesi za usajili magazeti ya Ulaya leo Jumatatu
Meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane amemwita Isco kusaini mkataba mpya ndani ya Bernabeu.
Nyota huyo Mhispania mkataba wake wa sasa utafikia ukingoni msimu ujao na ameonesha dalili za kutaka kuondoka huku klabu nyingi kutoka Premier League zikionesha nia ya kumnasa, lakini sasa Zidane amevuruga mipango hiyo.
"Ninataka aongeze, ni mchezaji muhimu," alisema Zidane.
"Anataka kucheza hapa. Ninafurahia kiwango chake, sio kwa magoli pekee bali ni kwa anachokifanya kati kati ya mistari uwanjani, anapowasaidia wengine kufanya."
Hizi hapa habari nyingine zilizoteke magazeti ya leo Jumatatu
- Real Madrid wanatarajia kufanya usajili kwa nyota wawili wakubwa ndani ya VPL, mlinda mlango wa Manchester United, David De Gea na mshambuliaji wa Chelsea, Eden Hazard ambapo pia wapo tayari kumuuza Alvaro Morata katika kukamilisha dili hizo ambazo zinaweza kugharimu jumla ya pauni mil 100.
- Meneja wa Crystal Pallace, Sam Allardyce amesema kwamba itawabidi Tottenham Hotspurs kutoa dau la kutosha ili kumnasa winga Wilfried Zaha.
- Bournemouth nao wapo tayari kupambana na West Ham kwa ajili ya kumnasa Jack Wilshere kutoka Arsenal kwa mkopo msimu huu.
- Kiungo wa Paris-Saint Germain, Marco Verratti atafanya mazungumzo na klabu yake hiyo kuhusu hatma yake mwishoni mwa msimu huu huku tayari vilabu vya Barcelona, Chelsea, Manchester United na Juventus vikitajwa kuhusishwa nae.
- Nyota anayewindwa na Man City, Malcom ametolea nje uwezekano wa kuelekea Premier League baada ya kufunguka kua ana furaha ndani ya Bordeaux.
- Liverpool wanajipanga kumpatia mkataba mpya Dejan Lovren kabla ya kumalizika kwa msimu huu.
- Crystal Palace wanatizamiwa kumsainisha mkataba wa kudumu Mamadou Sakho majira ya kiangazi.
Real Madrid wamng'ang'ania Isco,, pia kuwasajili Hazard, De Gea.....tetesi za usajili magazeti ya Ulaya leo Jumatatu
Reviewed by Steve
on
Monday, April 03, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment