Propellerads

Baada ya kuumia huenda Zulu akakosa mechi na Waarabu



Baada ya kiungo wa Yanga, Justine Zulu raia wa Zambia kupata jeraha la ugoko, daktari aliyemtibu, Nassor Matuzya amefunguka kuwa kiungo huyo atakaa nje ya uwanja kwa siku saba hali ambayo inaweza kumfanya kuukosa mchezo ujao dhidi ya Waarabu wa Algeria, MC Alger.

Zulu alipata majeraha hayo katika mchezo wa juzi Jumamosi wa Ligi kuu Bara dhidi ya Azam baada ya kugongwa na kiungo wa Azam, Himid Mao, dakika ya 58 na kushindwa kuendelea na mchezo huo huku nafasi yake ikichukuliwa na Emmanuel Martin.

Akizungumza katibu wa chama cha Madaktari wa Tiba za Michezo Tanzania (Tasma), Matuzya ambaye pia amewahi kuwa daktari wa Yanga, amesema Zulu alipata michubuko miwili katika sehemu moja ya ugoko.

"Palepale uwanjani tulimshona nyuzi kumi na tunatarajia atakaa nje ya uwanja kwa takribani siku saba akiwa chini ya uangalizi maalum.

"Lakini ndani ya siku hizo, itamchukua kama siku tatu kabla ya kutolewa nyuzi ili aanze mazoezi mepesi, lakini jambo la kushukuru ni kwamba licha ya jeraha lenyewe kua kubwa, kitendo cha kumuwahi kimesaidia kupatikna kwa unafuu.

"Alikua amevaa kizuia ugoko, lakini ukiangalia Himid alimkwaruza na hajamkita, hivyo kiatu chake kimemchana kwa umbali wa sentimeta nne na nusu mpaka sita, na isingekuwa amevaa kabisa kizuia ugoko, basi jeraha lingekua kubwa sana," alisema Matuzya.
Baada ya kuumia huenda Zulu akakosa mechi na Waarabu Baada ya kuumia huenda Zulu akakosa mechi na Waarabu Reviewed by Steve on Monday, April 03, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.