TFF watoa msimamo juu ya tukio la Abdi Banda kwenye mechi na Kagera Sugar
Kufuatia beki wa Simba, Abdi Banda kumtandika ngumi kiungo mkongwe wa Kagera Sugar, George Kavila, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema kuwa litamuadhibu Banda endapo ripoti ya mwamuzi itaonesha kosa hilo.
Banda alifanya kosa hilo kwenye mchezo wao wa wikiendi iliyopita walipopoteza mbele ya Kagera Sugar kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera ambapo tukio hilo halikuonwa na mwamuzi wa mchezo huo lakini marudio ya kamera yalilionyesha dhahiri.
Akizungumzia tukio hilo, Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas, amesema kwamba hawawezi kufanya maamuzi yoyote ya kumuadhibu Banda mpaka kosa lake liainishwe kwenye ripoti ya mwamuzi wa mchezo huo ambayo itatua mezani mwa kamati ya saa 72 kujadiliwa.
"Sisi tunasubiri ripoti ya mwamuzi halafu Kamati ya saa 72 itakaa kufanyia maamuzi kwa matukio yote yaliyotokea kwenye mchezo ule.
"Lakini nye ya hapo tuna watu wetu ambao tuliwatuma na hao pia watatuandikia ripoti yao na kama wakiainisha tukio hilo basi tutachukua hatua stahiki dhidi yake," alisema Lucas.
TFF watoa msimamo juu ya tukio la Abdi Banda kwenye mechi na Kagera Sugar
Reviewed by Steve
on
Wednesday, April 05, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment