Propellerads

Tetesi: Beckham anataka kumshawishi Rooney nae ajiunge MLS



Magazeti ya Uingereza yamedai kua David Beckham ana
mpango wa kumvuta Wayne Rooney nae siku za usoni atue ligi ya Marekani   MLS.

Inadaiwa Rooney amekua akimtumia ujumbe wa simu Rooney kumtaka awemo katika timu yake mpya anayoianzisha itakayocheza kwa mara ya kwanza msimu wa 2018.

Kwa kipindi hicho mkataba wa sasa wa Rooney na Man United utakua umefikia mwisho  na huenda akaelekea Marekani.

Hata hivyo kamishna wa MLS,  Don Garber amekanusha kua wana mpango wowote na Rooney kutokana na sababu kua hataki kuingilia maslahi ya rafiki yake Glazers ambaye anamiliki Man United huku ikizingatiwa Rooney bado yuko kwenye mkataba nae .

Hata hivyo riupoti zinasema MLS wako tayari kumpokea kwa mkono miwili Rooney endapo ataamua kuja.

Ligi hiyo imekua ikivuta majina makubwa katika soka huku ikitarajiwa nyota wengine kama Rooney kujiunga pia na kina Steven Gerrard, Frank Lampard na Andrea Pirlo ambao wamejiunga majira haya ya joto.
Ungana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na tuffollow Twitter @Kandanda 24

Tetesi: Beckham anataka kumshawishi Rooney nae ajiunge MLS Tetesi: Beckham anataka kumshawishi Rooney nae ajiunge MLS Reviewed by Steve on Monday, September 14, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.