Hii hapa siri ya ushindi wa Yanga jana kutoka kwa Mkwasa
Kocha msaidizi wa Yanga Charles Boniface Mkwasa amesema,
kucheza vizuri kwa timu ya Coastal Union ndiko kulikowafanya wao waibuke na ushindi huku akiipongeza timu hiyo yenye maskani yake jijini Tanga kwa kiwango walichokionesha kwenye mchezo wao wa jana uliokuwa wa ufunguzi wa ligi kwa upande wa timu hizo ambazo hazikucheza siku ya Jumamosi.
“Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kupata matokezo mazuri na tulijipanga kuweza kupata magoli mengi zaidi lakini matokeo yametokea tumepata magoli mawili, kutokana na nafasi ambazo tulizitumia vizuri kipindi cha kwanza” amesema Mkwasa.
“Lakini niwapongeze Coastal Union wamecheza vizuri na kucheza kwao vizuri ndio kumetupa sisi ushindi na sasa kilichaosalia ni kujipanga kwa ajili ya mchezo wa Jumatano maana mchezo huu tayari umeshakuwa ‘history’”.
“Matarajio yetu ni kufanya vizuri, mwaka jana timu haikuanza vizuri, mwaka huu tulitaka kuanza vizuri, na kama tumeanza vizuri basi tutajipanga na mechi zinazofata tufanye vizuri lakini najua kila mechi itakuwa ngumu lakini tutajitahidi ili tuweze kufanya vizuri zaidi”.
Hii hapa siri ya ushindi wa Yanga jana kutoka kwa Mkwasa
Reviewed by Steve
on
Monday, September 14, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, September 14, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment