Samatta shujaa Stars ikiichapa Botswana.
Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mbwana Samatta amedhihirisha kwamba hakupewa cheo hicho kwa bahati mbaya, baada ya jana kuisaidia timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Botswana, mabao yote yakitoka mguuni mwake.
Samatta anayekipiga katika klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji, alifunga mabao hayo katika mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya wapinzani wao hao, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam.
Samatta aliandika bao la kwanza katika dakika ya pili ya mchezo kutokana na pasi nzuri kutoka kwa Ibrahim Ajib, ambapo goli hilo lilidumu mpaka kipindi cha mapumziko.
Bao la pili alitupia dakika ya 87 katika kipindi cha pili kwa mkwaju wa faulo ambapo ulienda moja kwa moja wavuni hivyo mpaka mwisho wa mchezo Stars 2 na Botswana wakiwa bila bao lolote.
Samatta shujaa Stars ikiichapa Botswana.
Reviewed by Steve
on
Sunday, March 26, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment