Propellerads

Wilshere kuondoka Arsenal, Yaya Toure nae mkataba wake unaelekea ukingoni....stori za usajili kutoka magazeti ya Ulaya Jumapili ya leo



Jacky Wilshere yupo tayari kuachana na Arsenal na kuelekea AC Milan, hii ni kwa mujibu wa Daily Mail.

Kiungo huyo alikua akikipiga kwa mkopo Bournemouth katika harakati za kujiweka sawa, kwa sasa amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake na Gunners.

Hizi hapa 'Top Stories' nyingine kutoka magazeti ya Ulaya Jumapili hii:


  • Manchester City wapo katika nafasi kubwa ya kumsajili Danny Rose huku Luke Shaw akielekea Spurs.

  • Arsenal wamelenga kumnasa mlinda mlango wa Leicester, Kasper Schmeichel.

  • Endapo Liverpool watafanikiwa kucheza Klabu Bingwa Ulaya, basi milango ya kumsajili nyota wa Real Madrid, James Rodriguez itakua wazi kabisa.

  • Leicester wapo macho juu kwa Demarai Gray kwa dau la pauni mil 12 huku Liverpool, Everton na Spurs nao wakionesha nia.

  • Mahasimu wa AC Milan, Inter Milan wanajiandaa kuweka dau la pauni mil 20 kwa ajili ya nyota kutoka Tottenham, Moussa Sissoko.

  • Valencia wanataka kubadilisha mkopo wa Eliaquim Mangala kutoka Man City na kumchukua jumla jumla katika mkataba wa kudumu majira ya joto.

  • Huku mkataba ukielekea mwishoni mpaka kufikia majira ya joto, Yaya Toure amekua katika mipango ya vilabu vya Milan (Inter na AC) na Monaco.



Wilshere kuondoka Arsenal, Yaya Toure nae mkataba wake unaelekea ukingoni....stori za usajili kutoka magazeti ya Ulaya Jumapili ya leo Wilshere kuondoka Arsenal, Yaya Toure nae mkataba wake unaelekea ukingoni....stori za usajili kutoka magazeti ya Ulaya Jumapili ya leo Reviewed by Steve on Sunday, March 26, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.