Propellerads

Morata kutua Chelsea, Navas nae kurejea Sevilla....hizi hapa stori za usajili magazeti ya Ulaya leo Jumatatu




Alvaro Morata aweka wazi anataka kuondoka Real Madrid huku kocha wa Chelsea, Antonio Conte akidaiwa kutaka kumnasa katika kikosi chake Stamford Bridge.

Morata alijiunga na Real Madrid akitokea Juventus msimu uliopita majira ya joto ambapo hata hivyo amejikuta akipata nafasi mara chache kuanza na kikosi cha kwanza.

Conte anaonekana kua na uhitaji mkubwa kwa mshambuliaji huyo Mhispania, kwani kwa mujibu wa AS inadaiwa amemsisitiza tajiri Roman Abramovich kua inahitajika kiasi cha pauni mil 56 mezani ili kumnasa.

Mbali na habari hiyo, hapa chini ni 'top stories' nyingine kutoka magazeti ya Ulaya leo


  • Jack Wilshere anaweza kuelekea AC Milan endapo Arsene Wenger ataendelea kua kocha wa Gunners.

  • Winga wa Manchester United, Jesus Navas amehusishwa na kutaka kurejea klabu yake ya zamani ya Sevilla.

  • Manchester United wanaweza kumsajili Marcelo Brozovic majira ya joto ambapo kiungo huyo wa Inter Milan anaweza kununuliwa kwa pauni mil 40.

  • Pamoja na msimu mbaya chini ya kocha Arsene Wenger, Olivier Giroud bado ana imani ndani ya kikosi cha Arsenal.

  • Mkongwe wa Liverpool,  Terry McDermot amethibitika kwenda kufanyiwa upasuaji baada kupata mshtuko Disemba mwaka jana.



Morata kutua Chelsea, Navas nae kurejea Sevilla....hizi hapa stori za usajili magazeti ya Ulaya leo Jumatatu Morata kutua Chelsea, Navas nae kurejea Sevilla....hizi hapa stori za usajili magazeti ya Ulaya leo Jumatatu Reviewed by Steve on Monday, March 27, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.