Propellerads

Yanga wanawahitaji Ajibu na Mkude, uongozi Simba wafunguka mengi, lakini kikubwa ni kwamba...




Kufuatia tetesi zilizojitokeza hivi karibuni kuwa uongozi wa Yanga upo katika mipango ya kuwachukua wachezaji wa Simba, kiungo Jonas Mkude na mshambuliaji Ibrahimu Ajibu, mabosi wa wachezaji hao wameibuka na kusema kuwa ni ruksa kwa kuwa wachezaji hao wapo huru kufanya chochote kutokana na mikataba yao kuelekea ukingoni.

Kuna taarifa kuwa tayari kuna mipango imeanza kufanywa ndani ya Yanga kuhakikisha wanawapata wachezaji hao kutokana na majina yao kutajwa kuwepo katika mchakato wa kusajiliwa msimu ujao wa ligi kuu kufuatia mikataba yao kumalizika huku Ajibu akitajwa kuwa katika rada zao kwa muda mrefu.

Mwenyekiti wa kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema kuwa iwapo kuna watu wanafanya mazungumzo na wachezaji hao waendelee kwa kuwa hawawezi kuwazuia sababu ni wachezaji huru ambao mikataba yao inakaribia kumalizika.

"Kama kuna watu wanafanya nao mazungumzo waache tu waendelee kuzungumza nao, mimi sijui chochote, watu wamekuwa wakiniuliza sana kuhusiana na jambo hilo, kwa upande wetu muda bado wa kuweza kuzungumzia swala hilo, ila tunachojua bado ni wachezaji wetu na hawajamaliza mikataba yao hadi mwisho wa ligi.

"Kwa sasa Ajibu na Mkude ni wachezaji huru popote wanaweza kwenda kama Yanga wamefanya nao mazungumzo ni sawa, kwani mchezaji akiwa anakaribia kumaliza mkataba anakuwa huru hivyo ni ruksa kuzungumza na timu nyingine kusema watu wa Yanga wanawahitaji mimi hainihusu na wala siwezi kuwazuia, ni ruksa kwenda kokote.

"Kwa sasa mtazamo wetu wote ni wenye ligi na tutakapofikia huko tutasema kinachoendelea, wakati wa usajili bado," alisema Hanspope.
Yanga wanawahitaji Ajibu na Mkude, uongozi Simba wafunguka mengi, lakini kikubwa ni kwamba... Yanga wanawahitaji Ajibu na Mkude, uongozi Simba wafunguka mengi, lakini kikubwa ni kwamba... Reviewed by Steve on Monday, March 27, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.