Drogba na sababu za kuondoka pia hatma yake baada ya Chelsea.
Mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba amethibitisha kua ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu, na amefafanua kua ni wapi anaelekea baada ya
Stamford Bridge.
Drogba ambaye msimu huu amefanikiwa kuchukua taji la nne la Premier League akiwa na Chelsea, amedai kua bado anafikiria ni Ligi gani anaweza kwenda miongoni mwa ligi kubwa ulimwenguni.
Drogba aliulizwa kua kama anaweza kwenda ligi ya Marekani kama ikitokea akapata mkataba mnono huko.
Mkongwe huyo wa Chelsea amedai kukosa namba ya kudumu klabunindio sababu iliyomfanya aondoke, lakini anaamini kua kuna wachezaji vijana wengi ambao nao pia ni muda wao kung'aa.
"Niliongea na Jose (Mourinho) na bodi, na wote tukafikia mwafaka" Drogba aliongeza.
"Kiukweli nahitaji kuendelea kucheza zaidi, kabla sijaacha soka napenda nifaidi kwanza kwa kupata muda wa kutosha uwanjani.
"Kwa hiyo mimi kuendelea kukaa halafu nimalize sina furaha, hiyo haitawezekana , kwa hiyo tulielewana na kukubaliana kipi chenye manufaa kwetu pande zote,
"Pia nadhani na timu inahitaji kua imara zaidi msimu ujao, kushindana klabu bingwa, na wananunua wachezaji wapya. Pia kuna chipukizi anbao nao wanahitaji kucheza
"Sio kwamba naogopa ushindani nao, ila naodhani ni muda wa kuwapa nafasi nao pia"
Drogba na sababu za kuondoka pia hatma yake baada ya Chelsea.
Reviewed by Steve
on
Wednesday, May 27, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, May 27, 2015
Rating:
