Tetesi za usajili Arsenal.
Arsenal wameripotiwa kutafuta saini za wachezaji watatu katika dirisha lijalo la usajili, ambapo wanahitaji golikipa, kiungo na
mshambuliaji.
The Gunners muda mrefu wamekua wakihusishwa na kipa chaguo la pili wa Chelsea Petr Cech , lakini pia kulingana na ripoti zinadai Artulo Vidal au Morgan Schneiderln mmoja kati yao anaweza kuchukuliwa, na pia kati ya Karim Benzema au Jackson Martinez nao ni miongonimwa wanaowindwa kuimarisha kikosi.
Kwa Cech bado mpaka sasa haijathibitika kama ataondoka Stamford Bridge msimu huu na pia ukizingatia kama ni rahisi kwa Mourinho kumuuzia hasimu wake mkubwa Wenger.
Katika upande wa kiungo, kuna wachezaji Artuo Vidal wa Juve na Schneiderln ambao kila mmoja anaonekana kufaa zaidi kuipa nguvu Arsenal upande wa kati.
Ripoti kutoka Chile zinadai kua Vidal atajiungana The Gunnerrs kwa dau la pauni mil. 25 baada ya kombe lijalo la Copa America, huku upande wa Schneiderlin ambaye anawindwa na Wenger muda mrefu yeye amedai anataka kucheza klabu bingwa-kwa maana anahitaji usajili timu itakayocheza UEFA.
Olivier Giroud anaonekena kuelemewa upande wa mbele, hivyo Arsenal inatafuta mshambuliaji mwingine atakayeongeza nguvu katika safu hiyo,
Tetesi za usajili Arsenal.
Reviewed by Steve
on
Wednesday, May 27, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, May 27, 2015
Rating:
