Propellerads

Wakala wa Cristiano Ronaldo katika mazungumzo na Man United & Chelsea.


                                      

Kama ilivyoripotiwa kufukuzwa kwa kocha wake, Real Madrid pia wanaonekana kua katika hali tete kidogo, Jose Mendes amefanya mazungumzo na vilabu vya
Manchester United na Chelsea kuhusu upatikanaji wa Ronaldo.

Kulingana na mwandishi mmoja wa Hispania, Alfredo Duro, Mendes alipanda ndege mpaka Manchester ambako hakuishia kufanya mazungumzo ya De Gea pekee, bali pia kuhusiana na Ronaldo.

Duro amethibitisha kua mazungumzo kati ya Mendes na Man U hayakuwa kwa ajili ya De Gea pekee, bali pia uwezekano wa kumpata Ronaldo.

"Jose Mendes alipokua Manchester hakuzungumzia De Gea pekee, lakini pia upatikanaji wa Ronaldo" Duro aliiambia Marca Radio.

Tetesi juu ya Man U kumhitaji Ronaldo zimepungua sana kipindi hiki ambapo klabu pia imeonesha nia ya kumsajili Gareth Bale.

Bado haijafahamika kama endapo kocha Louis Van Gaal atamchukua nani kati ya Ronaldo au Baleambao hali ya sasa klabuni Madrid inaonekana kua tete.
Wakala wa Cristiano Ronaldo katika mazungumzo na Man United & Chelsea. Wakala wa Cristiano Ronaldo katika mazungumzo na Man United & Chelsea. Reviewed by Steve on Wednesday, May 27, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.